In Summary
  • Muigizaji Brian Ogan almaarufu Luwi afihua matapeli waliokuwa wanatumia jana lake kutapeli wakenya
  • Aliwashukuru wakenya kwa kufichua matapeli hao huku akisema hao wtakuwa mfano mwema
OGANA

Muigizaji wa kipindi cha Maria Brian Ogana almaarufu Luwi Hausa kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewafichua matapeli ambao wamekuwa wakitumia jina lake kuwatapeli watu.

Luwi alisema kwamba amewaripoti matapeli hao kwa DCI ili waweze kuchukuliwa hatua kwa kuibia wakenya wasio na hatia kupitia jina lake.

Tapeli huyo alijaribu kumuomba muigizaji huyo msamha ilgali nguvu zake ziliambulia patuu kwa maana Briana alimwambia anapaswa kutumia jasho lake kupata riziki na wal si kutumia majina au jasho la mtu mwingine.

 

Huku akiamba msamaha tapeli huyo alikiri kwamba hakuwa na kazi ndio maana alifanya hayo.

Pia aliwashukuru wakenya na mashabiki wake kwa kuafichua matapeli hao na kuwaambia wazidi kutuma namba za matapeli ambao wamezoea kuibia wakenya.

"Lowa jasho ili kupokea kilicho chako, wacheni kutumia njia za mkato kwa kuwadanganya watu tunawakujia nyinyi matapeli wote 

Huyu atakuwa mfano mwema, asanteni sana mashabiki endeleeni kutuma namba za matapeli hao." Luwi Alisema.

Tapeli huyo aliahidi kwamba hatorudia kitendo hicho tena.

View Comments