In Summary
  • Msanii Koffi Olomide kufanya collabo na staa wa bongo Diamond
  • Msanii huyo alimsifia Diamond na kuwaambia mashabiki wake wawe tayari kwa kibao moto moto
Koffi Olomide na Diamond Platnumz
Image: Hisani

Awali kumekuwa na uvumi kuwa staa wa bongo Diamond Platnumz amekuwa na maongezi na msanii wa nyimbo za Rhumba Koffi Olomide ili waweze kushirikiana katika kibao kipya.

Sasa mambo yamekuwa ya kweli hii ni baada ya Olomide kufichua haya kwenye mitandao yake ya kijamii huku akimsifia Diamond na kusema kuwa hawatawaangusha mashabiki wao.

Baada ya msanii Olomide kuwasili alikuwa kwenye mahojiano na kusema kwamba anapenda nyimbo zake Diamond na alipenda kufanya kazi naye ambapo ndoto yake imetimia.

Awali msanii huyo hajakuwa akiwashirikisha wasanii wenzake kwenye vibao vyake vipya.

"Tayari tuko studioni kuwafanya mjihisi vyema na mzuri na @Diamondpltnumz hamtavunjika mioyo Boss ya mboka." Aliandika Olomide.

Mtu mwenye bahati ni producer wake Diamond ambaye atakuwa producer wa kwanza kuzalisha kibao chale Koffi Olomide katika Afrika mashariki.

 

 

 

 

View Comments