In Summary
  • Sababu ambazo wakristo wengi hawafanikiwi maishani
church beer 5

Kulingana na utafiti idadi kubwa ya  wakristo hawafanikiwi maishani kwa ajili ya sababu moja au nyingine.

Kuna  wale ambao wamefanikiwa maishani na wale ambao wanag'ang'ana katika maisha yao ya kila siku.

Kuna wale  ambao wamekaa  bila kazi na hawajui kesho itakuwa vipi na waptakimu aje  mahitaji yao, swali ni je! nani ya kulaumu, hao wenyewe au wametelekezwa na Mungu wao?.

 
 

Katika makala haya tutazungumzia sababu ambazo wakristo wengi hawafanikiwi maishani na kubaki kuwa watu wa omba omba.

Hizi hapa baadhi ya sababu hizo;

1.Uvivu

Kuna baadhi ya wakristo ambao wana uvivu wa kuenda kutafuta kazi na kupata riziki yao ya kila siku.

Hata katika kitabu cha Methali chasema asiyefanya kazi na asile, lakini wengi wanaamini kuwa Mungu ndiye atakaye leta mafanikio bila kutia bidii hapo ndipo wengi wamekosea.  

2.Dhambi

Kuna wale watafanya dhambi na kisha kuomba msamaha wanapoenda kanisani, wakitoka kanisani wanarejea kutenda dhambi na katika imani ya wakristo wanajifungia baraka.

3.Kuchanganyikiwa na kukosa msimamo

Wengi hawajui waende kanisa lipi, wakisikia muhubiri yule anafanya miujiza anakimbia hapo na kutoka kanisa ambalo alikuwa anashiriki.

Wakati wao mwingi wanaharibu wakihama hama makanisa eti wanatafuta miujiza ya kupata utajiri.

4. Roho ya kutoamini

Wengi wakipata shida na kupitia milima na mabonde wanakata tamaa ya kutafuta riziki ya kila siku na kisha kutoamini tena.

Kwanini usimuamini Mola kwa kila jambo, usikimbilie utajiri au jambo ambalo hujui mwanzo na mwisho wake.

Wenye imani husema wakati wa Mungu ndio bora zaidi kuliko wa mwanadamu yeyote yule.

Wakristo wanapaswa kutia bidii zaidi huku wakiendelea kumuomba Mungu ili wafanikiwe maishani mwao. 

Kumbuka mgaa gaa na upwa hali wali mtupuu.

(Mhariri: Davis Ojiambo)

View Comments