In Summary
  • Tanasha Donna afichua hatarudi Tanzania hivi karibuni bali atampa yaya wake mtoto waende kumtembelea Diamond
Tanasha

Msanii n babay mama wa Diamond Tansha Donna harudi Tanzania hivi karibuni hii ni baada ya kusema haya akiwa kwenye mahojiano.

Akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hatorudi huko bali atampa yaya wake mwanawe waende pamoja kumtembelea baba yake Diamond.

"Sitarudi huko tena labda nitampa yaya wangu mwanangu waende pamoja, lakini kwangu mimi nimeshikana na mambo yangu humu nchini." Tanasha Alisema.

 

Usemi wake Tanasha unajiri wiki chache baada ya Zari Hassan kuwapeleka wanawe kumuona baba yao baada ya Diamond kumaliza miaka miwili bila ya hata kuwaona wanawe.

Pia usemi wake unajiri siku moja baada ya Diamond kudai kwamba anajivunia sana kubarikiwa na watoto wakiwa na Zari.

Diamond aliweza kumsifia Zari na kusema kwamba huyo ndiye mzazi ambaye anaweza kumsifia kati ya baby mama wake wote.

Zari alipowasili nchini Tanzania alisema kwamba hajarudiana na Diamond bali amewapeleka wanawe kumuona baba yao.

View Comments