Ommy Dimpoz ajiunga na lebo ya Sony Music Africa huku akitoa kibao chake cha 'Dede'
- Ommy Dimpoz atoa kibao kipya baada ya kujiunga na lebo ya Sony Music
Msanii wa Tanzania Omary Nyembo almaarufu Ommy Dimpoz amejiunga na rekodi ya lebo ya kimataifa Sony Music Africa.
Habari hizo zilitangazwa na meneja wa msanii huyo Seven Mosha.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram pia msanii huyo alisema kuwa ana furaha tele kujiunga na lebo hiyo.
Ommy anajiunga na wasanii kama vile Alikiba, Redsan na miongoni mwa wasanii wengine.
Msanii Ommy anatarajiwa kutoa albamu mpya mwaka mapema mwaka ujao huku wimbo wake akiutoa siku ya Alhamisi.
Ni kibao ambacho kimepokewa vyema na mashabiki.
Huu hapa ujumbe wake msanii huyo;
"NINAYO FURAHA KUJIUNGA NA MY NEW FAMILY @sonymusicafrica siwezi ngoja kuachilia albamu yangu mpya mapema mwaka ujao Dude letu la kwanza kutoka kwenye Album #DEDE tunaliachia leo Saa 10 jioni subscribe on my Vevo Channel link on Bio Chiiiiiiiiiiiii!!!!!!" Aliandika Ommy
Mashabiki walimpongeza Ommy Dimpoz kwa kazi yake nzuri, hii hapa video hiyo;
The video could not be loaded.