In Summary
  • Kutoka kwa Massawe hadi kwa Wahu:Watu mashuhuri waliomtetea kanze Dena baada ya kukejeliwa na wanamitandao
  • Haya yalitokea siku ya Ijumaa baada ya Kanze kuhotubia wanahabari katika ikulu ya Sagana

Bada ya wanamitandao kujitokeza na kumkejeli Kanze Dena kwa ajili ya kuongeza uzito, watu mashuhuri balimbali walijitokeza nao kidete na kusimama na Kane Dena.

Wengi wao walilaani kitendo hicho, huku wakisema kwamba ni jambo ambalo halikustahili kufanyika.

Mtangazaji wa Radiojambo Massawe Japanni alikuwa miongoni mwa watu ambao walikashifu kitendo hicho.

Massawe aliandika haya;

"Tutaweza kuwa aje katika kiwangi cha chini?kumkejeli mtu kwa ajili ya kuongeza uzito?haujui wala kufahamu anachopitia mtu huyo,"

Pia msanii Wahu hakuachwa nyuma pia naye alikashifu kitendo hicho kwa ujumbe huu;

"Ni aibu kubwa kuona watu kwanza wanawake, wakimkejeli mwanamke kwa ajili ya kuongeza uzito hasa wakati ametoka kujifungua,tunaweza kuwa bora,wacheni tuwe bora,"

Pia mtangazaji Joyce Gituro alisema,

"@kanzedena254 , you are a child of God, wonderful creation of the almighty, ignore the naysayers!”

DJ Soxxy naye aliwakashifu wanamitandao na kusema kwamba kila mtu alizaliwa na mwanamke ambaye alibadilika baada ya kutuzaa.

"Kwa nini mtu amkejeli KanzeDena kwa ajili ya kuomgeza uzito, sisi sote tulizaliwa na akina mama ambapo maisha yao yalibadilika baada ya kutuzaa."

Miongoni mwa watu wengine mashuhuri ambao walimtetea Kanze Dena ni pamoja na Terence Creative,Emmy Kosgei miongoni mwa wengine.

 

View Comments