In Summary
  • Staa wa bongo Diamond Platnumz ametangaza kurejeshwa kwa runinga ya Wasafi baada ya kufungwa miezi miwili iliyopita
  • Wasafi TV ilipigwa marufuku kwa miezi 6 lakini walizingatia tena adhabu hiyo na kupunguza marufuku kuwa miezi 2
Diamond

Staa wa bongo Diamond Platnumz ametangaza kurejeshwa kwa runinga ya Wasafi baada ya kufungwa miezi miwili iliyopita.

KUpitia kwenye ukurasa wake Diamond wa Instagram alitangaza habari hizo njema kwa mashabiki wake.

Runinga ya Wasafi ilipigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mwanzoni mwa mwaka 2021 baada ya kosa kufanywa dhidi ya kanuni zinazohitajika.

Β 

Walirusha maonyesho na Gigy Money ambaye kulingana na mamlaka, hakuwa mzuri.

Wasafi TV ilipigwa marufuku kwa miezi 6 lakini walizingatia tena adhabu hiyo na kupunguza marufuku kuwa miezi 2.

Runinga hiyo itarejeshwa tarehe 1 Machi 2021.

Hizi baadhi ya hisia za wanamitandao baada ya Diamond kupakia habari hizo;

tanashanation: Tv πŸ“Ί LETU LINARUDIIII TENA πŸ”₯πŸ™ŒπŸ”₯πŸ™Œ

wcb_updater: Wanalalamika material yamepotea so unawasidiaje πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

mamajamimu: Wasije wakasema caption c ya kiheshima wakaongeza cku bassataπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Β 

n.a.s.h.y_el_shakty: Simbaaaaaaaaaaa

lj__china_tz_store: Chombo kwa hewa

View Comments