In Summary
  • Bahati awaambia mashabiki kwamba ni ndugu yake Willy Paul
bAHATI 1

Miaka chache iliyopita tumeshuhudia msanii Bahati na Willy Paul wakiwa na ugomvi, huku wote wakitoka kwenye tasnia ya nyimbo za injili.

Mnamo Alhamisi wawili hao kupitia kwenye kurasa zao za instagram walipakia picha na Video ambapo walikuwa wanataniana.

Baada ya Bahati kupakia picha hiyo aliwashauri mashabiki wake wasidanganywe na mitandao ya kijamii, bali wwili hao ni ndugu.

 

"Niko hapa Nauliza Willy Paul Ni Nini ilikua inamkasirisha Nikishinda Groove Awards??? 🤣🤣🤣 Msi danganyike na mitandao ya kijamii...sisi ni ndugu🤝🤝🤝," Aliandika Bahati.

Pia alimsifia Willy Paul na kusema kwamba hajaweza kumpata mtu mwingine ambaye amempenda vile msanii Pozze anampenda.

Wawili hao walikuwa na msanii mwenzao DK Kwenye Beat.

“Guys I Just Noticed if I was a Woman Mtu wa Kwanza Ningepea ni Mg Brother Pozzee ...Sijawahi patana na mtu mwingine ambaye ananipenda kama vile anavyonipenda🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ukweli au Uongo???”

View Comments