In Summary
  • Katika jumbe kadhaa kwenye ukurasa wa twitter, DCI ilimtaja Obare kama Msaliti wa udanganyifu
  • Huku wengi wakitaka aachiliwe, aliyedaiwa kuwa mpango wa kando wa mcheza santuri DJ Mo mwaka jana, kupitia kwenye ukrasa wake wa instagram alifurahi kukamtwa kwa mwanablogu huyo
Egdar Obare
Image: DCI

Wapelelezi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) walitoa taarifa ya kina kuthibitisha kukamatwa kwa mwanablogu Edgar Obare na mshtakiwa mwenzake Desy Oduor Achieng.

Katika jumbe kadhaa kwenye ukurasa wa twitter, DCI ilimtaja Obare kama Msaliti wa udanganyifu ambaye amekuwa akiajiri wanawake wadogo kufuata watu maarufu katika duru za kisiasa, biashara na dini kwa unyonyaji wa pesa.

Kulingana na DCI Obare alikuwa amemfunza Desy jinsi ya kutapeli gavana mmoja humu nchini kwa udai kuwa na mtoto naye la sivyo ataambia ulimwengi kuwa ana mtoto nje ya ndoa

Pia idara hiyo ilisema kwamba gavana huyo hakujibu jumb zao.

KUpitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter wanamitandao wametaka Obare kuachili huru.

Huku wengi wakitaka aachiliwe, aliyedaiwa kuwa mpango wa kando wa mcheza santuri DJ Mo mwaka jana, kupitia kwenye ukrasa wake wa instagram alifurahi kukamtwa kwa mwanablogu huyo.

Margaret aliandika na kusema kwamba hizo zimekuwa habari njema kwake.

"Habari njema ambazo nimesikia siku nzima," Aliandika Maragaret.

View Comments