In Summary
  • Orodha ya wanasanii wa Reggae walioaga dunia na watakumbukwa milele
  • Siku chache zilizopita tulimpoteza mmoja wa wasanii wa Reggae na alikuwa rafiiki wa karibu wa Bob Marley
Image: BBC

Kifo ni jambo ambalo halipendwi na wanadamu wengi, lakini licha ya hayo yote kila dakika, sekunde na kila siku kuna wale waaga dunia wakati wao ukifika.

Katika makala haya tunazungumzia wasanii wa nyimbo za Reggae ambao waliaga dunia lakini nyimbo zao zinawafanya wengi wawakumbuke milele.

Siku chache zilizopita tulimpoteza mmoja wa wasanii wa Reggae na alikuwa rafiiki wa karibu wa Bob Marley.

Soma orodha ya wasanii hao;

1.Lucky Dube

Kupitia kwa nyimbo zake, msanii huyo hukumbukwa kila wakati hasa na mashabiki wa nyimbo hizo

Mnamo Oktoba mwaka wa 2007 msanii huyo aliuawa na majambazi akiwa Johannesburg.

2.Bob Marley

Pia ni msanii ambaye naye anafahamika sana kupitia kwa nyimbo zake,Dube aliaga dunia akiwa na miaka 36, Mei 1981.

3.Gregory Isaacs

Msanii huyo aliaga dunia mwaka wa 2010 Oktoba.

4.Bunny Wailer

Wailer ndiye msanii wa awali wa Reggae ambaye ameaga dunia, msanii huyo aliaga tarehe 2 Machi 2021, baada ya kuugua kwa muda.

Mungu na azidi kuzilaza roho zao mahali pema peponi.

 

 

 

 

View Comments