Msanii Loise Kim alaumu vipaza sauti kwa kusambaza virusi vya corona miongoni mwa wahubiri na wasanii
- Msanii Loise Kim alaumu vipasa sauti kwa kusambaza virusi vya corona miongoni mwa wahubiri na wasanii
- Usemi wake ulijiri saa chache baada ya mwandishi wa habari katika kampuni ya Royal Media Robin kuaga dunia kutokana na virusi hivyo
Msanii wa nyimbo za kikuyu Loise Kim kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alilaumu vipasa sauti kwa kusambaza virusi vya corona miongo mwa wahubiri, wasanii na hata wanahabari.
Usemi wake ulijiri saa chache baada ya mwandishi wa habari katika kampuni ya Royal Media Robin kuaga dunia kutokana na virusi hivyo.
Pia usemi wake ulijiri baada ya muhubiri maarufu na msanii wa nyimbo za kikuyu Mercy waciama kuaga dunia iliyodaiwa aliaga dunia kutokana na virusi hivyo.
Ni mwaka mmoja tangu kisa cha kwanza cha virusi vya covid-19 kutangazwa nchini, huku zaidi ya watu elfu moja wakiangamizwa na virusi hivyo.
Kulingana na msanii huyo wasanii wengi wanaoaga dunia kutokana na virusi hivyo ni kwa ajili ya vipasa sauti ambavyo wanatumia wakiburudisha mashabiki wao.
"Wahubiri na waimbaji wengi wameshindwa na mnyama huyu,Nadhani vipasa sauti ni bingwa katika usambazaji wa corona Ikiwa haijasafishwa vizuri tunaweza kuishia kuwapoteza wengi Kwaya za kanisa, wakuu wa sherehe, wanahabari na kadhalika jilindeni ni utafiti wangu," Alisema.