In Summary
  • Mastaa wa bongo fleva kutoka Tanzania wamtolea Magufuli vibao,wakimsifu
  • Wakati wa kampeni ya Magufuli mwaka jana aliwaleta wasanii wa bongo pamoja huku asilimia kubwa ya wasanii hao wakimpigia kampeni

Dakika chache baada ya tangazo la kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli, wasanii wa Bongo Flava wakiongozwa na Diamond, Juma Jux,Zuchu na Khadija Kopa walienda studio kurekodi wimbo maalum wa heshima kwa Rais wao aliyeondoka.

Video zilipakiwa kwenye mitandao ya kijamii na idadi kadhaa ya vyombo vya habari vya hapa Tanzania, inachukua wanamuziki zaidi ya 20 katika studio katikati ya usiku, ikimsifu Magufuli kupitia utunzi maalum.

Wakati wa kampeni ya Magufuli mwaka jana aliwaleta wasanii wa bongo pamoja huku asilimia kubwa ya wasanii hao wakimpigia kampeni.

 

Kibao cha kumsifu Magufuli cha wasanii wa lebo ya wasafi kinatarajiwa kutolea leo.

Wakati huo huo msanii Rayvanny ametoa kibao akisifu uongozi wake mwendazake Magufuli.

Rayvanny kupitia kwa kibao chake alisema kwamba nuru ya Tanzania imepotea, kufuatia kifo chake Magufuli.

Pia aliuliza ni nani atakaye futa machozi na mkewe Magufuli na pia watanzania wote kwa jumla, msanii huyo alisema kwamba Magufuli aliwapenda wasanii.

Rayvanny pia alisema kwamba rais huyo ameacha alama na kumbukumbu ambayo haitawahi futika.

Hii hapa video ya kibao hicho;

The video could not be loaded.

Follow Rayvanny On: Twitter : http://www.twitter.com/rayvanny/ Facebook : https://www.facebook.com/RaymondVanny/ Instagram : http://www.instagram.com/rayvanny/ For Bookings: Email: rayvanny@wcbwasafi.com
Pia Msanii Harmonize alitoa kibao huku akimuomboleza Magufuli, na hii hapa video ya kibao chake'

The video could not be loaded.

Konde Gang For Woldwide https://youtu.be/vW3aZIpCbP8 https://youtu.be/4692FxBUP40 https://yt.be/artistinsights/vngpm2CcQLP3EjwYA contact : kondegang12@gmail.com +1 5053150647 Copyright ©2021 KONDE MUSIC WORLDWIDE .All rights reserved.

 

 

 

 

View Comments