In Summary
  • Msanii Willy Paul awaonya wanawake ambao wanatumia jina lake kupata umaarufu
Willy Paul

Msanii Willy Paul amewaonya wanawake ambao wanatumia jina lake ili kupata umaarufu, kulingana na msanii huyo alifanya bidii kuwa mahali alipo leo.

Pia alisema kwamba kama hampendi mtu, hakuna kitu ambacho kinaweza fanyika na anajua jinsi kukataliwa inaumwa.

UJumbe wake Willy ni wa wanawake ambao wamekuwa wakitafuta kiki kwa jina lake huku wakisema kwamba wana ujauzito wake na mwishowe wanabadilisha hadithi yao.

Paul alisema kwamba mwaka huu ni wa mabadiliko kwake,na mtu yeyote atakaye cheza naye asimulaumu kwa matokeo.

KUpitia kwenye ujumbe wake alisema kwamba amewasamehe wote ambao walimkosea heshima.

"Wanawake wanawake wanawake, tafadhali mambo hayalazimishwi sawa ??? Kwa hivyo ikiwa sikupendi sijakupenda !! Na ikiwa haunipendi haunipendi !!!

Kwa hivyo tafadhali tusilazimishe maswala. Najua wakati mwingine  kukataliwa ni ngumu. Hii inatumika kwa pande zote mbili, hata hivyo, leo nataka kuweka wazi kitu ......

Nimefanya bidii zaidi kufikia hapa nilipo. Sikuamka tu siku ya Jumapili nikajikuta hapa. Mimi nilifanya kazi kwa bidii

Naona nimekua lengo ya kila msichana mwenye kudai kuwa maarufu, swali ni kwanihuu umaarufu uko na nini? Aaaai !!! 2021 ni mapinduzi tu na kusafisha fujo ..

kwa hivyo mtu yeyote ambaye atajaribu ujinga asini alaumu mimi. Ninakataa kuwa njia rahisi ya mtu kutoka. Pambana na hali yako ufike penye utaweza .. kwa wale wameshajenga mastory zikatokea nimekusamehe. Kwa wale wanapanga, kila la kheri 😆 tupatane mbele!"

 

 

 

 

 

 

View Comments