In Summary
  • Sonko awashauri wakenya kufanya haya ili kupigana na corona
  • Kisa cha kwanza cha virusi vya covid-19 mwaka jana 2020, Machi
Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko

Huku maambukizi ya corona yakizidi kuongezeka kila siku na hata watu kupoteza maisha yao kila kuchao wakenya wanaendelea kushauriwa kufuata kanuni za wizara ya afya.

Kisa cha kwanza cha virusi vya covid-19 mwaka jana 2020, Machi.

Aliyekuwa gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook amewashauri wakenya kufuata na kuzingatia kanuni za wizara ya afya.

 

Pia aliwakumbusha kumwambia Mungu awalinde kama vile huwalinda siku hizo nyingine.

"Watu wangu ukiweza kila siku jaribu kuchukua mchanganyiko wa maji moto, limao, tangawizi na vitunguu saumu na kama uko na Pesa ununulia virutubisho nyongeza ya kinga ya mwili ambayo husaidia katika kusafishamapafu yako na maambukizo yoyote

Mbali na kunawa mikono na kuvaa barakoa na kukaa umbali wa mita moja unahitaji kuweka mwili wako ukiwa na afya njema. Mwishowe kumbusha Mungu kukukinga kama vile hufanya kila wakati. Nakutakia Jumapili njema."Sonko Aliandika.

Je swali kuu unajikinga na unafuata kanuni za wizara ya afya ili kupigana na janga la corona au wachulia kila kitu mzaha?

View Comments