In Summary
  • Staa wa bongo Diamond Platnumz akizungumza baada ya kuona mwili wa hayati rais John POmbe Magufuli, alisema kwamba mwendazake alikuwa kama baba yake

Staa wa bongo Diamond Platnumz akizungumza baada ya kuona mwili wa hayati rais John POmbe Magufuli, alisema kwamba mwendazake alikuwa kama baba yake.

Hii ni kwa sababu alikuwa anasumbuka na changamoto ambazo wasanii walikuwa wanapittia na wanchi wa Tanzania kwa jumla.

Msanii huyo alisema kwamba Magufuli  atakumbukwa daima milele na watanzania.

 

Pia alifichua kwamba alipokuwa amezingirwa na drama ya nani baba yake mzazi miezi chache iliyopita Magufuli alimpigia simu na kumjulia hali.

Kikubwa ni kuendelea kufanya vitu ambavyo alivizungumza vile vyema lakini pia waaminisha vijana na watanzania kuwa kila kitu kinawezekana…katika muda wake aliongoza amefanya vitu vingi sana kwa hivyo inaonyesha kuwa tunaweza. Alipokuwa anasema Tanzania ni Tajiri sio kwamba hela iko mfukoni ila tuina resources ambazo tukitumia vizuri itatupa maendeleo.

Ukaribu wake ulikuwa mkubwa kwa Jamii maana wakati mwingine unaweza kuwa umekaa alafu Rais anakupigia simu mnazungumza kama mtu unaongea na mzazi wako. Na hata kipindi kile yalipotokea maswala ya Baba alinipigia simu kuniuliza. Kwa hiyo ni mtu ambaye tutamkumbuka kwa vitu vingine. Alikuwa anatumia muda mwingi kufanya kazi ili tupate maendeleo,"Alizungumza Diamond.

Diamond alisema kwamba anamuamini rais mpya wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Suluhu.

Suluhu aliapishwa siku ya Ijumaa, Machi 19 kuwa rais wa Tanzania na rais.

 

 

 

 

View Comments