'Kimbia dhambi ya ngono,'Msanii Size 8 awaelimisha shabiki kuhusu dhambi ya ngono
- Msanii wa nyimo injili Size 8 amekuwa akiwaelimisha mashabiki wake kuhusu biblia na ndoa kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram
Msanii wa nyimo injili Size 8 amekuwa akiwaelimisha mashabiki wake kuhusu biblia na ndoa kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram.
Wiki iliyopita alizungumzia jinsi Mungu amemuwezesha katika ndoa yake licha ya kukumbana na changamoto.
Siku ya Ijumaa Size 8 aliwaelimisha mashabiki wake kuhusu dhambi ya ngono, huku akiwashauri wanapaswa kukimbia kutoka kwa dhambi hiyo kwani inahusisha mwili wa mwanadamu.
"KImbia kutoka kwa dhambi ya ngono, hamna dhambi nyingine ambayo uhathiri mwili kama hii,kwa usherati hii ni dhambi dhidi ya mwili wako
Je haufahamu kuwa mwili wako ni hekalu ya roho mtakatifu ambaye anaishi ndani yako aliyeletwa kwako na Mungu
Wewe si mali yako mwenyewe, kwani Mungu alikununua kwa bei ya juu, kwa hivyo unapaswa kumheshimu Mungu na mwili wako," Aliandika Size 8.
Je unamheshimu Munu na mwili wako, na unafahamu kuwa mwili wako ni hekalu yake mwenyezi Mungu?