In Summary
  • Flaqo awaonya mashabiki dhidi ya kutuma picha wakiwa uchi
flaqo-324x235

Mchekeshaji Flaqo, ni mmoja wa wachekeshaji ambao wameinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kwa ajili ya bidii yao.

Kupitia kwenye ukuras wake wa instagrm Flaqo aliwauliza mashabiki wa kiume na kike wawache kutuma picha zao wakiwa uchi kwani hawajui kesho yao.

Watu wengi haswa akina baba zetu wanaogopa kuingia kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya picha kama hizo.

 

Wiki jana msanii Akothee aliwaonya wanaume ambao wamekuwa wakimtumia picha wakiwa uchi, huku akiweka bayana kwamba amekuwa akiogopa kuingia kwenye DM yake kwa ajili ya picha hizo.

Ujumbe ake Flaqo uliwaendea vijana ambao wamekuwa wakitishia kufichua picha za wanawake wakiwa uchi ambazo wamekuwa wakiwatumia.

"KUna kesi nyingi ambazo zimekuwa zikiongezeka awali vijana wakitishia kufichua picha za wasichana wakiwa uchi 

Hii ni baada ya kutokubaliana na jambo fulani, na kuwatapeli na pesa, kuweni makini wanawake na wanaume

Wacheni kutuma picha mkiwa uchi au nyenzo ambazo zitakuweka kwa shida kwa maana hujui kesho yako wacheni kutuma picha mkiwa ucho ovyo ovyo

na muache kupigana au kutishiana kwa ajili ya pesa jameni, utu," Aliandika Flaqo.

 

 

 

 

 

 

View Comments