In Summary
  • Akothee awajibu watanzania kuhusu Forbes
  • Mwanamuziki huyo tokea Tanzania aliwasihi Forbes kufanya utafiti dhabiti kabla ya kuweka jina lake kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika
akoth

Wiki iliyopita staa wa bongo, Diamond Platnumz alisuta kampuni ya Forbes baada ya kumweka kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Mwanamuziki huyo tokea Tanzania aliwasihi Forbes kufanya utafiti dhabiti kabla ya kuweka jina lake kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Katika video ambayo imeenea sana ya msanii wa Tanzania Baba Levo,Akothee ameiona na kuwajibu watanzania kuhusu Forbes huku akiwaambia hana pesa wala ushirirkiano na Forbes.

Katika orodha hiyo Akothee alikuwa amemshinda Diamond kwa utajiri kama msanii.

KUlingana na Baba Levo, wanamuziki kutoka Nigeria ndio walitengeneza orodha hiyo na ilikuwa bandia.

Hayo sio makosa ambayo alifanya bali, makosa ambayo alifanya ni kumtaja Akothee, aiwa kwenye mahojiano hayo.

Kwa haraka Akothee naye alimjibu kwa ujumbe huu;

"Eeee hii kitu ya Forbes imekuwa Kesi Bongo 🤔🤔🤔.Kisa Akothee , kwani Mimi tu ndio msanii alikuwa Kwenye hiyo list 🤣🤣🤣,

Kwani mumesikia niko na shares Forbes 🙈 hata hamnaa Aibu jamani ,si watu wajiheshimu kidogo.Akothee mwanamke anawatishia hivi,

haya basi Mimi sina kitu sina hata matako tuu.Yaishe Yaishe ,Yaishe .wacheni kutembea Kwenye vyombo vya jabari na jina la LE PREZIDATHE PRESIDENT OF SINGLE MOTHERS. Wakenya wamenichoka , hivi bongo nikija itakuwaje 🤔🤔🤔🤔," Aliandka Akothee.

KUpitia kwenye ukurasa wa twitter wa msanii Alikiba alimsihi Diamond awache kulalamika, kwani waliotoa orodha hiyo wana maarifa zaidi.
View Comments