In Summary

•Alisema kuwa alisikitishwa sana na matamshi ya Mutuana kusema kuwa anatumai kuwa suluhu itapatikana hivi karibuni.

•Kufuatia hayo, Khaligraph aliahidi kuanzisha mashindano ya muziki ya wiki mbili ambapo shilingi nusu milioni zitashindaniwa.

Image: HISANI

Mwanamuziki tajika wa nyimbo za kufoka nchini Kenya Khaligraph Jones amemkosoa mkurugenzi mtendaji wa  Bodi ya Filamu na Uainishaji nchini Kenya (KFCB) Ezekiel Mutua kwa kile amesema ni kutoheshimu talanta za wasanii wa Kenya.

Khaligraph alikuwa anadondoa matamshi ya Mutua dhidi mcheshi Eric Omondi kuwa yeye ni maskini na anapenda kiki. 

Alisema kuwa alisikitishwa sana na matamshi ya Mutuana kusema kuwa anatumai kuwa suluhu itapatikana hivi karibuni.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki huyo alipakia video ya kikejeli ambapo alishika mabunda ya pesa alizodai kuwa laki tano ili kuonyesha kuwa kwa kweli talanta inalipa.

Kwenye video hiyo, Khaligraph alishika mabunda matano ya laki moja moja kila bunda, akayawekelea kwenye sikio lake la kulia na kuigiza kama kwamba anampigia Omondi simu akiwa Tanzania.

"Kuna habari imenifikia, kuna kitu niliona kwa mneti kuna gathee anasema ati wasanii wako hali mbaya, wasanii wote wamechapa. Alikuwa anawaambia mbaya mazee, alikuwa anaambia Eric Omondi. Kwa hivyo nataka kumpigia Eric Omondi aniambia kama hii stori ni ukweli mazee niskie form ni gani. Kwa nini wasanii wanabebwa ndogo hivo" Khaligraph alisema kabla ya kuchukua pesa zile na kujifanya anapiga simu.

Kwenye video nyingine alishauri Wakenya kusita kuwadhalilisha wasanii 

Jones alimwambia Mutua kuwa ni jukumu lake kupatia motisha wasanii chipukizi na kuwashauri kuhusiana na jinsi ya kukuza talanta zao badala ya kuwatusi na kuwadhalilisha.

Kufuatia hayo, Khaligraph aliahidi kuanzisha mashindano ya muziki ya wiki mbili ambapo shilingi nusu milioni zitashindaniwa.

Khaligraph pia aliahidi kupatia wasanii watatu chipukizi mkataba wa kurekodi mziki katika studio yake ya Blu Ink Corp.
View Comments