In Summary

•Msanii huyo alisema kuwa hakuwa ametenda kosa lolote dhidi ya Alai wakati aliamua kumshambulia kwa rungu.

•Alidai kuwa alikuwa amelala hospitalini na alikuwa na maumivu tele kichwani na kwenye mkono.

•Alihimiza taasisi za kulinda sheria kuhakikisha kuwa sheria imefuatwa kila wakati.

Image: INSTAGRAM//RINGTONE APOKO

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Ringtone Apoko amewasili katika mahakama ya Kibera kushudia mwanablogu Robert Alai akisomewa mashtaka ya shambulio aliyomshtaki nayo.

Kwenye video iliyoenea sana mitandaoni Ijumaa wiki iliyopita, Ringtone na Alai walionekena kusababisha drama barabarani huku msanii huyo akiwa amesimama juu ya gari lake aina la Rangerover akiwa anamtetesha Alai kwa kile alisema ni kuchukua sheria mikononi. Apoko alionekana kuvunja damu kwenye upande wa kichwa chake.

Ringtone ambaye alionekana kuwa na maumivu  aliwasili mahakamani akiwa amebebwa na gari la kubebea wagonjwa. 

Msanii huyo aliyekuja kutambulikana sana kutokana na kibao chake 'Pamela' alikuwa na bendeji mkononi na kwenye kidevu chake.

Alipokuwa anahutubia wanahabari nje ya mahakama, mwanamuziki huyo alidai kuwa alikuwa na maumivu tele kwenye kichwa na mkono wake na alikuwa ametoka hospitani baada ya kulala huko.

"Mimi naumwa! Mwili wangu hauko sawa. Mimi sikuwa mgonjwa" Ringtone alidai.

Msanii huyo alisema kuwa hakuwa ametenda kosa lolote dhidi ya Alai wakati aliamua kumshambulia kwa rungu.

"Mimi sikumkosea Robert Alai na aliamua tu kunivamia. Nilipandisha kioo ya gari wakati alikuja kunitukana. Yeye akaona akuje na rungu apasue kioo ya gari. Akavunjavunja na akanifikia na akaniumiza," Aliendelea kusema.

Alihimiza taasisi za kulinda sheria kuhakikisha kuwa sheria imefuatwa kila wakati.

"Ile siku mimi Ringtone nitaenda nivamie mtu, nataka tu sheria itumike... nashangaa kwa nini kesi yangu inaendelea tu kuzungushwa.. Nataka kuambia Wakenya wa kawaida tusipoteze matumaini. Bado naamini Kenya ni nchi ambayo ninafuata sheria, ata kama ni mtu mkubwa ama mdogo, ukikosea mwenzako kwa kumpiga lazima sheria itatumika" Alisema Ringtone.

Mwanamuziki huyo alidai kuwa yeye hajawahi kuwa mtu wa vurugu na hajawahi kumpiga yeyote.

"Mimi sijawahi julikana kumpiga mtu, huwa sipigani. Hii mambo yote huwa tunafanya kwa mtandao ni kutumbuiza tu. Lakini mambo ya vurugu, sijawahi kumpiga mtu. Nataka kumuomba Inspekta Jenerali wa polisi na DPP watumie tu sheria ya Kenya," alisema.

View Comments