In Summary
  • Msanii na mwanabiashara Akothee amekuwa akivuma kwa muda sasa baada ya kufichua maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi
  • Madam Boss ambaye matendo yake ya hivi karibuni kwenye mitandao yameashiria kuwa huenda wanachumbiana na Nelly Oaks aliyekuwa meneja wake ameendelea kumbubujikia sifa si haba
Esther Akoth

Msanii na mwanabiashara Akothee amekuwa akivuma kwa muda sasa baada ya kufichua maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi.

Madam Boss ambaye matendo yake ya hivi karibuni kwenye mitandao yameashiria kuwa huenda wanachumbiana na Nelly Oaks aliyekuwa meneja wake ameendelea kumbubujikia sifa si haba.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee amedai kwamba umaarufu ulimnyima uhuru wake kwa muda.

"Kwa wale ambao wamekuwa wakiuliza kwanini sijakuwa na walinzi,  ni makosa yangu kwa sababu wakati mwingine walinzi wangu hawajui jinsi ya kukaa nami

Wakati mwingine nitaamka nataka kuwa peke yangu,kuhisi uhuru wakati mwinine wa kujiendesha, kujisikia kama mwanadamu wa kawaida

Nimecoka kuchungwa, kwani nimeiba nini ya watu, nichungwe kama mali ya serikali, umaarufu ulikuwa umeninyima uhuru wangu

Mambo yatakuwa sawa tena?" Aliandika Akothee.

View Comments