In Summary
  • Willy Paul awaonya waliomletea maumivu maishani mwake
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Msanii Willy Paul amekuwa akivuma sana kwa muda baada ya kutoa kibao chake huku akimshirikisha msanii wa nyimbo za injili Size 8.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo aliwaonya wote ambao wamekuwa wakimuobea mabaya, na kuwaambia kwaba siku zao zimehesabiwa.

Kulingana na Paul kuna wakati utafika atoe ushuhuda kwa ajili ya maisha yake.

"Kwa wale waliniletea maumivu maishani mwangu siku zenu zimehesabiwa,kwa wale walifanya na wanafanya maisha yangu yawe magumu pia siku zenu zimehesabiwa," Aliandika Willy Paul.

Pia msanii huyo amesema kwamba siku moja aatapeana hadithi yake na itakuwa ya ukweli mtupu.

"Siku moja nitasema hadithi yangu, na itakuwa ukweli mtupu, kwa muda mefu nimejiekea mambo moyoni mwangu lakini siweki tena

Jambo la mwisho nimekusudiwa ukuu,"

View Comments