In Summary

•Huku kesi kuhusiana na kifo cha mtoto huyo wa pili wa mfanyibiashara mashuhuri Tabitha Karanja, Anerlisa amepuuzilia mbali madai kuwa kifo cha dadake kilitokana na ajali.

•Binti huyo wa mmiliki wa Keroche Breweries amesema kuwa anaelewa kwamba dadake aliangamia mikononi ya mwuaji.

Anerlisa Muigai na marehemu Tecra Muigai
Image: HISANI

Anerlisa Muigai ambaye ni dada ya mrithi wa Keroche Tecra Muigai aliyefariki katika hali tatanishi mwaka wa 2020 hajapona kutokana na majonzi ya kumpoteza dada yake.

Huku kesi kuhusiana na kifo cha mtoto huyo wa pili wa mfanyibiashara mashuhuri Tabitha Karanja, Anerlisa amepuuzilia mbali madai kuwa kifo cha dadake kilitokana na ajali.

Anerlisa alipakia picha za kumbukumbu za marehemu dadake  na kueleza jinsi anampeza.

Kulingana na Anerlisa, Tecra hakuanguka kutoka kwa ngazi kama inavyodaiwa bali aliuliwa kikatili.

"Sitawahi kusahau kifo cha dadangu kwani najua vizuri kuwa hakuanguka kwa ngazi. Kitu kimoja ambacho watu hawafahamu ni kuwa alikuwa amevunjika mfupa mgumu zaidi mwilini wa binadamu. Mfupa huo waweza tu vunjwa na vitu viwili; ajali ya barabarani ama kugongwa na mtu kwa kifaa butu" Anerlisa alisema.

Anerlisa ambaye alikuja kufahamika zaidi wakati alikuwa anamchumbia mwanamuziki Ben Pol kutoka Bongo pia amepuuzilia mbali madai kuwa dadake alikuwa mlevi chakari wakati alikumbana na kifo chake.

"Dadangu hakuwa mlevi, na kama alikuwa amelewa alikuwa na ufahamu wa yale yote yaliyokuwa yanaendelea. Hakuwa amefikia kiwango cha kutojifahamu" Alisema Anerlisa.

Binti huyo wa mmiliki wa Keroche Breweries amesema kuwa anaelewa kwamba dadake aliangamia mikononi ya mwuaji.

"Dadangu aliuliwa kikatili!" Alimalizia kwa kusema.

Tecra Muigai alifariki mnamo Machi 2020  alipokuwa anapokea matibabu jijini Nairobi baada ya kuugua majeraha mabaya akiwa Lamu.

Upasuaji wa mwili ulidhihirisha kuwa marehemu aliangamia kutokana na majeraha aliyokuwa amepata kichwani.

View Comments