In Summary
  • Eric Omondi akejeliwa baada ya kumpendekeza Jimi Wanjigi kuwa rais wa Kenya
Eric Omondi
Image: Hisani

Baada ya Mchekeshaji Eric Omondi kumpendekeza bilionea Jimi Wanjigi kuwa rais wa Kenya mwaka baada ya kustaafu kwa Uhuru Kenyatta mwaka ujao,wanamitandao wamemkejeli na kutoa hisia tofauti.

Kupitia kampeni iliyobandikwa jina 'Fagia wote', Eric amesema kuwa wakati umewadia kwa wale wote ambao wamekuwa uongozini kwa miaka mingi kuenda nyumbani na kuachia viongozi wapya usukani.

"Hatutaki majina zinajulikana. 2022 tunawafagia wote. Vijana tumeamka na tunakuja" Omondi alisema kwenye video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Omondi amesema kuwa kinara wa ODM Raila Odinga, naibu rais William Ruto, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzao wa ANC Musalia Mudavadi wameshindwa kusukuma nchi mbele na kuwataka wasiwanie viti hivyo mwaka ujao.

Hizi hapa baadh ya hisia za mwanamitandao;

karenzo.nyamu: Eric piga hustle. I hope amekulambisha fiti ama tumuanike πŸ˜‚πŸ˜‚

ngash4real: Hapo kwa Jimmy Wanjigi ndio umeanguka na tumbo

xclusivedeejay: So vijana we should rely on a 60 year old billionaire to help us ?? πŸ€¦πŸΏβ€β™‚οΈπŸ€¦πŸΏβ€β™‚οΈπŸ€¦πŸΏβ€β™‚οΈ vijana kweli tunapangwa tu kama kawa

charles_ndolo: πŸ˜‚πŸ˜‚ nilikuwa nafikiria kuna kitu ya maana mpaka nikafika hiyo part ya endorsement

kevinsky9: 😍so wanjigi or whatever his name is ni youthπŸ˜‚πŸ˜‚..enyewe uko na jokes.

babashawnpoetry: Ama unaadvertise kampuni ya vifagioπŸ™Œ

mariahkibs: Okay seriously??I thought kijana ni wewe.

ndungu_tosh: Jimi wanjigi amekuangushia kakiru mzuri sanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

masila_justus: Kufagia iko sawa ,lakini hapo kwa jimmy wajingo ndio nguvu imeishia

sammykham: Kijanaa amelipwa πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

View Comments