In Summary

•Jamaa kutoka Machakos ambaye alitambulishwa kama Justin Kioko 31, alidaiwa kujifanya kuwa mwanamke na kulaghai jamaa mwingine kutoka Siaya aliyetambulishwa kama Godfrey Owino shilingi 344,000.

•Kelvin Kinuthia alitumia ukurasa wake wa TikTok kupuuzilia mbali madai hayo huku akieleza kwamba picha zake zilitumika na mwanablogu kutafuta kiki.

•Kinuthia amekanusha madai kwamba kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi na kuwaonya wanablogu dhidi ya kutumia jina ama picha zake kueneza propaganda

Image: TWITTER

Moja kati ya habari ambazo ziliangaziwa sana mitandaoni siku ya Jumatatu ni kuhusu jamaa anayedaiwa kula nauli ya shilingi 344,000 ambayo alitumiwa na jamaa mwingine aliyedhani kuwa yeye ni mwanamke mrembo.

Ripoti moja ambayo ilisambazwa sana mitandaoni ilisema kuwa jamaa kutoka Machakos ambaye alitambulishwa kama Justin Kioko 31, alijifanya kuwa mwanamke na akalaghai jamaa mwingine kutoka Siaya aliyetambulishwa kama Godfrey Owino shilingi 344,000.

Kulingana na ripoti hiyo, Owino alimtumia Kioko pesa zile ili aweze kulipa nauli ya kutoka Kilifi hadi nyumbani kwake Siaya, kununua vitu anazohitaji na kununua simu mpya.

Ilidaiwa kwamba baada ya 'Kioko' kupokea pesa zile kupitia Mpesa  lizitumia kwa mahitaji yake mwenyewe na hakuwahi fika kwa Bw Owino.

Hata hivyo, jamaa ambaye apicha zake zimetumika kwenye ripoti hizo amejitokeza na kukanusha madai hayo.

Kelvin Kinuthia alitumia ukurasa wake wa TikTok kupuuzilia mbali madai hayo huku akieleza kwamba picha zake zilitumika na mwanablogu kutafuta kiki.

Kinuthia alisema kwamba majina yake rasmi ni 'Kelvin Kinuthia' wala sio Justin Kioko' na hata yeye sio mzaliwa wa Machakos.

"Mimi siitwi Justin Kioko. Jina langu ni Kelvin Kinuthia. Hayo mambo ya Justin Kioko siyafahamu. Pili kwetu sio Machakos. Ukisema mimi ni Justin Kioko na eti nimetoka Machakos unadanganya. Mimi hata sio Mkamba, mimi ni Mkikuyu.

Hakuna pesa zilizotumwa kwangu, eti 344,000 za nauli. Watu wengi wataamini habari hiyo kwa kuwa nimenunua simu mpya. Hakuna mtu aliyeninunulia hiyo simu. Hiuo ni uvumi tu ambao unaenezwa na wanablogu" Kinuthia alisema.

Kinuthia amekanusha madai kwamba kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi na kuwaonya wanablogu dhidi ya kutumia jina ama picha zake kueneza propaganda

View Comments