In Summary

•Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema ni heri mwanamke aombe ashauri kutoka kwa mtu wasiyejuana badala ya kupatia marafiki wao nafasi ya kuharibu ndoa zao.

•Kulingana na Vera, marafiki wengi huwa wazuri na kushauriana kuhusu mambo mengine tofauti lakini sio kuhusu mahusiano, mafanikio na baraka.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika ameonya wanawake dhidi ya kuwaomba marafiki wao  ushauri kuhusu mahusiano.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kwamba wanawake huwa hawapatii marafiki wao ushauri wa dhati kwani wengi wao huwa na nia ya kuwaibia wenzao wapenzi wao.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema ni heri mwanamke aombe ashauri kutoka kwa mtu wasiyejuana badala ya kupatia marafiki wao nafasi ya kuharibu ndoa zao.

"Haijalishi jinsi mzozo kati yenu ulivyo mbaya, usiombe marafiki wako ushauri kuhusiana na mahusiano yako. Ni heri uombe ushauri mtu ambaye hamjuani kwa matatu, treni, ndege ama mkahawa. Uliza wageni ambao hawakujui na hawajui mume wako. Hao watakupatia ushauri wa dhati.

Lakini marafiki wako ambao hawana mchumba na wameona mkifurahia mapenzi yenu na  kutamani wangekuwa na mpenzi kama wako hapana!! usijaribu. Mtanishukuru baadae" Vera amewashauri wanadada.

Kulingana na Vera, marafiki wengi huwa wazuri na kushauriana kuhusu mambo mengine tofauti lakini sio kuhusu mahusiano, mafanikio na baraka.

Vera amewashauri wanawake kusuluhisha matatizo katika mahusiano yao na wapenzi wao wenyewe badala ya kukimbia kutafuta ushauri kwa marafiki wao.

"Usiulize marafiki wako kuhusu hatua utakayochukua. Hiyo ndio njia rahisi ya kupoteza mwanaume mzuri ambaye amefanya kosa ndogo ambalo laweza suluhishwa. Wote wanamtaka ni ile tu hawawezi kuambia. Wanasubiri mzozane, wakupatie ushauri eti umuache wengine wakiwa na matumaini ya kumchumbia punde baada yenu kutengana" Amesema Vera.

Amesema kwamba hata hivyo wanaume wengi hutafuta wanawake wazuri ambao wanaona mema kwao badala ya kuchukua marafiki wa aliyekuwa mpenzi wake.

"Usiwe mwanamke ambaye hawezi fikiria ama kujiamulia mwenyewe" Alisema Vera.

View Comments