In Summary
  • Kulingana na Nyashinski maambukizi hayo yalikuja kutokana na mazoezi makali kabla ya tukio hilo
Screenshot-from-2020-06-18-14_21_12

Rapa maarufu nchini Nyamari Ongegu, almaarufu Nyashinski, anasema anaweza kosa kuhudhuria  onyesho lake kwenye tamasha la 'Destination Africa Festival' ambalo muigizaji wa Nigeria Adekunle Gold ndiye msanii mgeni.

Nyashinski siku ya Ijumaa alisema amepata maambukizi ya koo ambayo yanatishia kupatikana kwake kutumbuiza kwenye onyesho hilo.

Kulingana na Nyashinski maambukizi hayo yalikuja kutokana na mazoezi makali kabla ya tukio hilo.

“Huyu anahitaji IMANI! Nimekuwa na wiki ya kusisimua na vipindi vikali vya mazoezi ya kujiandaa na tamasha za Destination Africa

Kwa bahati mbaya, jana nilipata maambukizi ambayo yameambukiza koo yangu ghafla na kutishia utendaji wangu,” aliandika Nyashinski kwenye hadithi zake za Instagram.

Rapa huyo, huku akiomba maombi kutoka kwa mashabiki wake, aliongeza kuwa anatarajia maonyesho mengine kwenye tamasha hilo.

"Tafadhali tafadhali niekeni kwa maombi yenu."

Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.

 

 

View Comments