In Summary

•Eric alikuwa ametoa wito kwa wasanii na waandishi wa habari washirikiane naye katika maandamano kuelekea bungeni kudai kuchezwa zaidi kwa sanaa ya Kenya na malipo bora kwa wasanii wakati wa tamasha.

•OCPD wa kituo cha Central Adamson Bungei amesema Omondi alikamatwa kwa kusababisha fujo nje ya bunge.

Image: INSTAGRAM.// ERIC OMONDI

Mchekeshaji  Eric Omondi anadaiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa alipokuwa anaongoza maandamano jijini Nairobi.

Msanii huyo asiyepungukiwa na drama anaripotiwa kutiwa mbaroni asubuhi ya Jumanne alipokuwa ameongoza kikundi cha vijana kuandamana nje ya bunge la kitaifa kurekebisha sekta ya muziki nchini.

Eric alikuwa ametoa wito kwa wasanii na waandishi wa habari washirikiane naye katika maandamano kuelekea bungeni kudai kuchezwa zaidi kwa sanaa ya Kenya na malipo bora kwa wasanii wakati wa tamasha.

Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa akivuma sana hivi karibuni anadai vituo vya burudani vicheze asilimia 75 ya muziki wa Kenya.

Kwenye video ambayo imeenezwa sana mitandaoni mchekeshaji huyo anaonekana akikokotwa na polisi akielekezwa kwenye gari lililokuwa limesubiri kumpeleka kituoni.

Omondi anaonekana kusita kuingia ndani ya gari ya polisina badala yake anapanda juu na kuanza kutahadharisha polisi waache kumshika.

OCPD wa kituo cha Central Adamson Bungei amesema Omondi alikamatwa kwa kusababisha fujo nje ya bunge.

"Hakuwa amefuata taratibu za kufanya maandamano. Hata hivyo tunampanga,” Bungei amesema.

Ndugu ya msanii huyo, Felix Omondi amethibitisha kukamatwa kwake huku akieleza kwamba anazuiliwa katika kituo cha Central.

View Comments