Sijawahi rithi chochote kutoka kwa mume wangu Ivan-Zari Hassan afunguka
- Ssemwanga alikuwa mfanyabiashara anayeheshimika kutoka Uganda aliyefariki mwaka wa 2017
Zari amesema hakuwahi kurithi chochote kutoka kwa marehemu mumewe Ivan Ssemwanga na kuongeza kuwa walichokuwa nacho wote wawili walikifanyia kazi.
Ssemwanga alikuwa mfanyabiashara anayeheshimika kutoka Uganda aliyefariki mwaka wa 2017.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Toke Makinwa kwenye mtandao wa Youtube ‘The Hassans’, Zari alisema;
“Tulipoungana tulikuwa na matamanio makubwa sana, nikimtazama alikuwa na uwezo mkubwa na aliponitazama aliona nguvu yangu.
Kwa hivyo tuliunganisha nguvu zetu zote mbili na kuunda himaya. Sijawahi kurithi chochote kutoka kwake. Kuna nyakati tuliendesha gari ambalo milango yake hata haikufunguka, lakini watu hawakujua hilo.
Lakini sasa mtu anapokuona unaweka Lamborghini wanasema 'alirithi," Aliazungumza Zari.
Mama wa watoto watano anasema wakati mwingine yeye hutumia muda mwingi kulea na kuendesha biashara zake kiasi kwamba ni nadra sana kuwa na mwanamume.
Hata hivyo alieleza kuwa haimaanishi hataki kupendwa.
"Nimechumbiana na watu kadhaa na wakati mwingine iliishia kutofanya kazi kwa sababu nilijitolea kwa kazi yangu na kwa watoto wangu. Nataka kutanguliza."
Aliendelea;
"Watoto wangu na biashara wananihitaji na lazima niamue wapi nitaweka nguvu zangu kwanza na ninapofanya baadhi ya wanaume wanadhani nina nguvu na kujitegemea na hawahitaji mwanaume.
Wanawake wenye nguvu wanahitaji wanaume. Inakuwa vigumu kuchumbiana unapokuwa huru. Watu hufikiri, 'Ohh 'anazeeka na hahitaji mwanamume'."
The video could not be loaded.