In Summary

•Mama huyo wa watoto watano alisema hakuweza kujumuika na wengine kusherehekea siku ya Jamhuri kwani tangu Jumamosi amekuwa katika kitanda cha hospitali.

•Mwanamuziki huyo alimshukuru sana mpenzi wake Nelly Oaks kwa kumuonyesha upendo na kusimama naye katika wakati huu mgumu. 

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri Esther Akoth almaarufu kama Akothee amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya kwa muda sasa.

Siku ya Jumatano msanii huyo mwenye umri wa miaka 41 alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufichua kuwa amelazwa hospitalini kwa mara nyingine.

Mama huyo wa watoto watano alisema hakuweza kujumuika na wengine kusherehekea siku ya Jamhuri kwani tangu Jumamosi amekuwa katika kitanda cha hospitali.

"Pole kwa kuwaweka sana. Hapa ndipo pamekuwa maskani yangu tangu Jumamosi. Hata siwezi kuinua kichwa changu leo, Mungu juu ya yote!" Akothee alitangaza kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha yake akiwa amelala katika kitanda cha hospitali huku akionekana kuwa mdhaifu.

Mwanamuziki huyo alimshukuru sana mpenzi wake Nelly Oaks kwa kumuonyesha upendo na kusimama naye katika wakati huu mgumu. 

"Mara ya tano nalazwa hospitalini na ako hapa nami @nellyoaks" Aliandika.

Wiki iliyopita binti wa pili wa Akothee, Rue Baby aliahirisha sherehe hafla ya kusherehekea kuhitimu kwake kutoka chuo kikuu ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika Jumamosi iliyopita, siku ambayo mwanamuziki huyo alilazwa.

Kipusa huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema hatua ya kuahirisha sherehe zake iliafikiwa ili kupatia mamake muda wa kupata afueni kwani alikuwa anaugua.

View Comments