In Summary
  • Alizidi na ujumbe wake na kusema kwamba badala ya kuona haya yote heri awape block
  • Akothee asema hajali kuhusu chuki kutoka kwa familia
akoth stylish 1 (1)

Esther Akoth almaarufu Akothee ni miongoni mwa wasanii maarufu nchini ambao wanafahamika sana kwa ajili ya bidii ya kazi yao.

Licha ya kuwa mwanamuziki ni mama ambaye amewalea watoto wake kwa maadili mema, na kuwafunza kujitegemea kimaisha.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alisema kwamba hajali kuhusu chuki kutoka kwa familia hata baada ya kuwasaidia.

"Kuna familia ambazo dada zako ni adui zako, kaka wanaweza kuuwana wakipata nafasi, wajomba na shangazi wanawachukia wapwa wao sana

Heri wasaidie watu wa nje, chuki nyingi katika familia zingine kwa nini."

Alizidi na ujumbe wake na kusema kwamba badala ya kuona haya yote heri awape block.

"Nashindwa baada ya kufanya hayo yote mtu mahali ana nguvu ya kunichukia, inaitwa chuki, na mimi mwenye sijali na kupa block ata hata sitajaribu kukaribia familia yako," Alisema Akothee.

 

 

 

 

 

View Comments