In Summary
  • Msanii Akothee amesikitishwa na jinsi vijana wa sasa wamebebwa na mitandao ya kijamii licha yao kuwa na maisha yao
  • Kulingana na msanii huyo maarufu mitandao ya kijamii ina msongo wa mawazo sana
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Kwa hakika mitandao ya kijamii, imeleta shinikizo nyingi kwa vijana wwa karne ya sasa huku, baadhi yao wakihitaji utajiri wa haraka kama vvilee walivyoona mitandaoni.

Msanii Akothee amesikitishwa na jinsi vijana wa sasa wamebebwa na mitandao ya kijamii licha yao kuwa na maisha yao.

Kulingana na msanii huyo maarufu mitandao ya kijamii ina msongo wa mawazo sana.

"Maisha ya mitandao ya kijamii yana mafadhaiko sana ! Bila haya mambo 10! Hakuna mtu atakufuata! Na pamoja na mambo haya yote, bado unalala njaa, nje ya mitandao ya kijamii, wale wanaofuata na kupenda hawatakulisha hata kidogo 😭😭😭😭😭 Aaaah uchungu," Aliandika.

Kupitia kwenye chapisho nyingine Akothee alisema kwamba kizazi hiki kinasikitisha na huo ndio ukweli, kisa na maana mitandao ya kijamii.

"Nimekichambua kizazi hiki na ukweli mchungu ni , "INASIKITISHA" Mtandao umewaweka wazi watoto wetu maisha laini kiasi kwamba wote wanataka kuwa na maisha laini bila kuyafanyia kazi 😔 Inasikitisha kwamba wengi wao wanaruka mchakato wa ukuaji ili tu kuruka na kutua kwenye sehemu ya kaburi la mapema! 

Wanakaa 24/7 wakitembeza simu zao, kutoka wassap hadi face book hadi tiktok hadi twitter hadi simu kutwa! Mambo wanayotazama ni uwekezaji wa miaka 30 wa watu wengine

Wanashindana na watu wenye umri wa kuwalea 😒 Wanazungumza juu ya unyogovu wakati mambo hayaendi kwao! Haloo, ni nini kimeweka ubongo wako kwenye kina/ mapumziko?"

View Comments