In Summary
  • Binti yake Akothee, Rue Baby amezua tafrani tena mtandaoni, baada ya kuamua kutangaza hadharani kuwa mnamo Februari 14
Rue Baby
Image: Hisani

Binti yake Akothee, Rue Baby amezua tafrani tena mtandaoni, baada ya kuamua kutangaza hadharani kuwa mnamo Februari 14, ambayo ni siku ya wapendanao, atamtambulisha rasmi mwanamume wake kwa umma, na. atampakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Yaani hii Nairobi mtu hawezi kuwa na marafiki kwa amani,nyinyi watu mnapaswa kutulia na kuketi mngoje na mje pole pole siku ya wapendana nitampakia mwanamume wangu mitandaoni," Rue Aliandika.

Rue Baby hajawahi kuweka uhusiano wake hadharani, na kwa miaka kadhaa watu walidhani kwamba alikuwa akichumbiana na mchekeshaji maarufu Mc Tricky  lakini Tricky alimtambulisha mpenzi wake kwa umma, na hivyo kumfanya madai ya kufikia mwisho.

Ngoja tusubiri siku ya wapendanao tuone mwanamume anayechumbiana au aliyeteka moyo wake Rue Baby.

 

 

View Comments