In Summary
  • Hili lilikuwa jibu lisilotarajiwa, tukikumbuka kwamba Vera na Otile waliachana vibaya sanabaada ya wawili hao kuamua kutemana na kukamilisha uhusiano wao wa kimapenzi
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mjasirimali na mwanasosholaiti maarufu  Vera Sidika amezua hisia tofauti mitandaoni, baada ya kukiri hadharani na kusema kuwa ikiwa Otile Brown yuko tayari au anataka. collabo na mumewe Brown Mauzo ataunga mkono kikamilifu collabo hiyo.

Hili lilikuwa jibu lisilotarajiwa, tukikumbuka kwamba Vera na Otile waliachana vibaya sanabaada ya wawili hao kuamua kutemana na kukamilisha uhusiano wao wa kimapenzi.

Ni kana kwamba Vera amepata furaha tena na labda alimsamehe Otile Brown ndiyo maana hajawahi kusema jambo lolote mbaya kumhusu.

Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kupitia kwenye insta stories kumuuliza iwapo ataunga mkono collabo kati ya Otile na mumewe Mauzo.

"Kama Otile Brown atataka kufanya collabo na mpenzi wako Brown Mauzo utaunga mkono collabo hiyo au la," Shabiki Aliuliza.

"Nitaunga mkono kwa asilimia 100, hamna kitu mbaya na hilo," Vera Alijibu.

 

View Comments