In Summary

•Otile Brown amewasihi mashabiki wake kumkumbuka katika maombi yao huku akiendelea kuuguza maumivu yanayomkabili.

•Takriban siku tano zilizopita mwanamuziki huyo alifanyiwa upasuaji katika hospitali moja jijini Nairobi.

Image: INSTAGRAM// OTILE BROWN

Siku chache tu baada ya kufanyiwa upasuaji, mwanamuziki mashuhuri Jacob Obunga almaarufu kama Otile Brown amewaacha mashabiki wake katika hali ya wasiwasi kutokana na chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii.

Kigogo huyo wa muziki wa kisasa ametoa taarifa fupi kuhusu afya yake akifichua kwamba  anashuhudia  maumivu makali sana mwili mwake.

Otile Brown amewasihi mashabiki wake kumkumbuka katika maombi yao huku akiendelea kuuguza maumivu yanayomkabili.

"Nina maumivu makali sana..ombeeni Obizee" Brown ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Takriban siku tano zilizopita mwanamuziki huyo alifanyiwa upasuaji katika hospitali moja jijini Nairobi.

Akifahamisha mashabiki wake kuhusu hayo, Brown alipakia video iliyoonyesha akiwa anasukumwa kutoka kwa chumba cha upasuaji huku  akiwa amelazwa kwenye kitanda cha wagonjwa.

"Ilienda vizuri" Brown aliandika chini ya video iliyoonyesha akiwa ameporea katika wadi huku akionekana mchangamfu.

Otile Brown hata hivyo hakueleza sehemu ya mwili wake ambayo ilifanyiwa upasuaji wala kilichokuwa kimemwathiri.

View Comments