In Summary

•Apoko alisisitiza kuwa Alai alimshambulia vibaya na kumwaibisha hadharani, jambo ambalo hajawahi kufanikiwa kukabiliana nalo hadi leo.

•Alisema kuwa moyo wake hauna kinyongo chochote kwa sasa na kudokeza kuwa  sasa ni jukumu la Alai kutafuta upatanisho.

Image: HISANI

Siku ya Jumanne mwanamuziki wa nyimbo za injili Ringtone Apoko alifika katika mahakama ya Milimani kuhudhuria kesi ambapo anamshtaki mwanablogu Robert Alai kwa kosa la shambulio.

Akihutubia wanahabari nje ya mahakama baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa mara nyingine, Apoko alisema kuwa hana uhasama wowote dhidi ya Alai kwa sasa na tayari amemsamehe.

Mwanamuziki huyo asiyepungukiwa na drama hata hivyo alisisitiza kuwa ni sharti kesi hiyo iendelee kulingana na sheria za nchi na haki ipatikane.

"Naamini mahakama ya Kenya itaweza kutoa hukumu ya ukweli. Mimi sina ubaya na mtu, nishasamehea moyoni. Hata hivyo lazima tufuate sheria" Apoko alisema.

Apoko alisisitiza kuwa Alai alimshambulia vibaya na kumwaibisha hadharani, jambo ambalo hajawahi kufanikiwa kukabiliana nalo hadi leo.

Alishikilia kuwa moyo wake hauna kinyongo chochote kwa sasa na kudokeza kuwa  sasa ni jukumu la Alai kutafuta upatanisho.

"Mimi nishasamehea kwa moyo  wangu lakini Bibilia inasema bisha utafunguliwa, itisha na utapewa" Alisema.

Ringtone amesisitiza kuwa aliathirika vibaya baada ya kushambuliwa na Alai na kudai kuwa bado anaendelea kupokea matibabu maalum.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 9 kwani mahakama haikuwa na kikao siku ya Jumanne.

View Comments