In Summary

•Bahati amewapa changamoto wanaume wengine walio kwenye ndoa baada ya kumzawadi mkewe kwa zawadi ya gari, shamba, nyumba.

•Amesema kuwa mwanaume wa aina kama ya mumewe huwa  tayari kufanya lolote ili kudumisha mahusiano.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwanablogu mashuhuri Diana Marua ameshindwa kabisa kuficha furaha yake katika kipindi hiki cha wapendanao baada ya mumewe Bahati kumsherehekea kwa zawadi tatu kubwa.

Katika kipindi cha takriban wiki  moja ambacho kimepita Bahati amewapa changamoto wanaume wengine walio kwenye ndoa baada ya kumzawadi mkewe kwa zawadi ya gari, shamba, nyumba.

Diana Marua amemshukuru sana mumewe kwa kumpa zawadi hizo na amemuomba Mola amjaalie baraka nyingi, utajiri na neema katika siku zote za maisha yake. 

"Wewe ni mwana wa Mungu aliyechaguliwa, umependelewa sana!! Naomba neema zake zikupate katika siku zote za maisha yako. Nakupenda Bahati" Diana alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Diana ambaye hivi majuzi alizindua taaluma yake ya muziki akijitambulisha kama rapa Diana B amemtaja mumewe kama mwanaume anapenda na kuthamini kila sehemu yake. 

Amesema kuwa mwanaume wa aina kama ya mumewe huwa  tayari kufanya lolote ili kudumisha mahusiano huku akiwashauri wanadada wengine kusubiri kupata mchumba kama huyo wake.

"Siku moja utakutana na mtu anayeabudu ardhi unayotembea juu yake. Usitulie mpaka umpate huyo mwanaume. Atakupenda na kuthamini kila kitu chako, atafanya kila awezalo ili asikupoteze. Usitulie chini ya hapo. Nimempata huyo mtu, Yeye ni mfalme wangu" Diana amesema.

Bahati na Diana wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka mitano na tayari wamebarikiwa na watoto wawili pamoja.

View Comments