In Summary
  • Diamond ni mwanamuziki ambaye amefahamika sana kwa ajili ya bidii ya kazi yake
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platnumz kupitia kwenye ukurasa wake wa amewatangazia mashabiki wake kwamba ataachia EP yake ya kwanza kabisa katika muziki.

Diamond ni mwanamuziki ambaye amefahamika sana kwa ajili ya bidii ya kazi yake.

Vibao vyake vimekuwa vikipokea zaidi ya watazamaji milioni kumi, Pia ni msanii ambaye anafahamika kwa ajili ya baba mama wake.

Safari ya muziki ya msanii huyo inafahamika na kutambulika na wengi, kwani alianza na mwanzo wa chini huku akiinuka siku baada ya siku.

Aidha msanii huyo aliwauliza mashabiki wake kutoa majina ya EP yake.

"YES! March 4th 2022 My first EP in Music Life... Guess the tittle?Tareh 04, 03 2022 EP ya kwanza katika maisha ya Muziki wangu... Unazani Tuuitaje?," Aliandika Diamond.

 

 

 

 

View Comments