In Summary
  • Ili kufurahisha, kuna uvumi kwamba anatarajia mtoto wake wa kwanza na rapper huyo
  • Uvumi huo ulichochewa zaidi baada ya kushiriki video iliyoonyeshaujauzito wa mtoto wake ambaye tayari alikua amekua
Juliani na mke wake Lilian Nganga
Image: HISANI

 Lillian Ng'ang'a amekuwa akivuma mitandaoni siku chache zilizopita kufuatia harusi yake ya siri na mpenzi wake, rapa Julius Owino almaarufu Juliani.

Ili kufurahisha, kuna uvumi kwamba anatarajia mtoto wake wa kwanza na rapper huyo.

Uvumi huo ulichochewa zaidi baada ya kushiriki video iliyoonyeshaujauzito wa mtoto wake ambaye tayari alikua amekua.

Wanamitandao waliitikia hili kwa njia tofauti, ikizingatiwa kuwa alikaa na Dkt Alfred Mutua kwa takriban miaka kumi, lakini hakupata mtoto naye.

Kwa wengine, hakuwa tayari kujitoa katika ndoa yake na gavana, sababu alijiruhusu kubeba mtoto wa Juliani licha ya kuwa wamekaa pamoja kwa miezi kadhaa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instaram Lilian amewashauri mashabiki wake wasiogope kuanza tena endapo wataanguka.

Pia alifichua vitu ambavyo aliwacha nyuma baada ya kutengena na gavana Mutua.

"Usiwahi ogopa kuanza tena kwani inafanya kazi,kama mpenda kusoma nilikuwa na vitu vingi nilipokuwa naishi

Mwaka jana nilipoanza maisha upya niliviacha nyuma kimakusudi kama mwanzo mpya kumaanisha kuacha nyuma yaliyopita

Lei nilipokuwa nachukua kitabu cha kusoma niligundua jinsi maktaba yangu yanakua," Aliandika Ng'ang'a.

 

 

 

View Comments