In Summary

•Mwanasiasa huyo ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka jana amemshukuru Mola kwa kumjalia mwaka mwingine wa kuishi licha ya changamoto zote zilizomkumba.

•Sandra amemtaja babake kama mtu anayempa msukumo mkubwa wa kimaisha huku akimshukuru kwa upendo mkubwa ambao amemwonyesha katika siku zote za maisha yake.

Image: INSTAGRAM// MIKE SONKO

Hivi leo (Machi 3) aliyekuwa gavana wa Nairobi Gideon Kioko Mbuvi almaarufu Mike Sonko anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Mwanasiasa huyo ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka jana amemshukuru Mola kwa kumjalia mwaka mwingine wa kuishi licha ya changamoto zote zilizomkumba

Maelfu ya wafuasi wake kutoka tabaka mbalimbali wameendelea kumsherehekea kwa jumbe nzuri za kheri za siku ya kuzaliwa.

"Licha ya masaibu yangu nastahili kuwa na furaha kama Mkenya mwingine yeyote. Leo ni siku yangu ya kuzaliwa na ningependa tu kumshukuru Mungu kwa kuniongezea mwaka mwingine katika maisha yangu. Nitakushukuru daima Mungu," Sonko amejisherehekea kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Binti ya mwanasiasa huyo Sandra Mbuvi ni miongoni mwa waliojumuika naye kusherehekea siku hiyo muhimu maishani mwake.

Sandra amemtaja babake kama mtu anayempa msukumo mkubwa wa kimaisha huku akimshukuru kwa upendo mkubwa ambao amemwonyesha katika siku zote za maisha yake.

"Baba mpendwa, kila mwaka siku hii inanikumbusha jinsi nilivyobahatika kuwa na wewe kama baba. Asante kwa kunipenda bila masharti na kwa kunifundisha nisikate tamaa wewe ni msukumo wangu mkubwa. Heri za kuzaliwa baba, nakupenda," Sandra aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Binti mkubwa wa mwanasiasa huyo, Saumu Mbuvi pia hajasalia nyuma katika kumsherehekea babake huku akimhakikishia kuhusu upendo mkubwa alio nao kwake.

View Comments