In Summary
  • Grace Ekirapa azungumzia safari ya ujauzito wake,afichua alipoteza mtoto wa kwanza
Grace Ekirapa na Pascal Tokodi
Image: Hisani

Mtangazaji Grace Ekirapa na mumewe Pascal Tokodi wanatarajia mtoto wao Aprili/27/2022 kama walivyothibitisha katika hafla moja.

Wawili hao waliweka hafla ya shukrani kwa ajili ya mtoto ambaye wanatarajia.

HUku akizungumzia safarii yake ya ujauzito Grace alisema;

"Huyu ni mtoto wetu wa pili, tulimpoteza mtoto wetu wa kwanza mnamo Juni. Ilikuwa ngumu...lakini tuko hapa tena na tunamshukuru Mungu," alisema.

Katika ujauzito wake wa pili, Grace alisema kuwa imemfanya awe na hisia.

Aliongeza kuwa amekuwa na hofu kidogo katika safari ya ujauzito.

"Kusema kweli, tulipogundua kuwa tuna mimba tena niliogopa sana. Nafikiri niko mpaka sasa. Kila nikivuta msuli mimi hulia kama kichaa. ...kila wakati siwezi kuamka kwa sababu mtoto bado yuko kwenye mshipa...nahisi kama ninapoteza tena,” Grace alisema.

Mama mtarajiwa alisema mume wake Pascal Tokodi amekuwa akimuunga mkono na imembidi kuinua miguu yake mara kadhaa.

Grace aliongeza kuwa ni hofu ya uzoefu wake wa kwanza ambao ulimfanya kuweka ujauzito huo kuwa siri kwa muda mrefu.

“Nakumbuka nilimkaribisha mtu kwenye kipindi akaja....hata hakunijua alikuwa nabii kutoka Uganda...alikuwa anatabiri...akanitazama na kuniambia ‘naona kijana’ .Nikamwambia aache...niliingiwa na hofu kwa sababu ilikuwa hewani.Sikutaka watu wafahamu hadi hatuwezi kuficha tena.Nilikuwa watu wakigundua na tunapoteza tena,”alisema.

 Pascal aliendelea kueleza kwamba walipoteza ujauzito mwaka jana.

"Kama alivyosema, imekuwa safari ngumu...tupo hapa sasa tunashukuru. Huyu ni mtoto wetu wa pili, tulimpoteza mtoto wetu wa kwanza mnamo Juni. Ilikuwa ngumu...lakini tupo hapa tena na tunamshukuru Mungu. . Tuna miezi 8 sasa...tunaenda kwa miezi 9...tunatumai kwa miaka mingi zaidi," Pascal alisema.

The video could not be loaded.

This day was beautiful in every way. we chose to have a very intimate gathering because we needed to share that beautiful day with people who have in one way or another held our hands through this journey. We had the amazing Mbogori fashions do our outfits, Beauty lounge was on point with the Make up, the gorgeous venue was; The Kentmere Club and the breath taking Decor was by Che-Dream Makers. Not to forget Mbela who captured the beautiful moments and put this video together. Special shout out to Our Family MC Chege we love you God bless you as you watch this video.
View Comments