In Summary

•Milly ameweka wazi kuwa Kabi amekuwa akimtunza vizuri katika kipindi cha takriban miezi minane ambacho amekuwa akibeba ujauzito wa mtoto wao wa pili.

Image: INSTAGRAM// MILLY WAJESUS

Mwanavlogu mashuhuri Millicent Wambui almaarufu Milly Wajesus amempongeza mumewe Peter Kabi kwa kusimama naye katika safari yake ya ujauzito.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Milly ameweka wazi kuwa Kabi amekuwa akimtunza vizuri katika kipindi cha takriban miezi minane ambacho amekuwa akibeba ujauzito wa mtoto wao wa pili.

"Hakuna siku ambayo nimejisikia niko peke yangu wakati wa ujauzito huu. Umekuwa nami kila wakati ukifanya mengi zaidi kunifanya nijisikie kama malkia. Nimejisikia kupendwa na kuthaminiwa kila wakati na hili silichukulii kuwa la kawaida. Mungu akubariki sana," Milly alimwandikia mumewe.

Mama huyo wa mtoto mmoja amefichua kwamba mumewe alimwandalia baby shower ya kufana kisiri bila kumwambia.

"Nilikuwa nimekata tamaa ya kuwa na 'baby shower' au kujipangia moja  mwenyewe kwa sababu ya jinsi nilivyochoka  na tarehe yangu ya kujifungua inawadia," Alisema Milly.

Alisema alishangazwa na kitendo cha mumewe kupanga hafla iliyofanikiwa katika muda mfupi uliokuwepo.

"Natumai hii inawahimiza wanaume wote huko nje kuchukua jukumu la kusherehekea malkia wao. Anastahili kusherehekewa kwa kubeba donge hilo kwa fahari," Milly alisema.

Kabi kwa upande wake alieleza furaha yake kuona kwamba mkewe ameridhishwa na hafla ambayo alimwandalia. Alifichua kwamba amepanga kumpa mkewe zawadi zingine saba.

View Comments