In Summary

•Mke huyo wa zamani wa gavana Alfred Mutua amesema watu kama hao kwa kawaida huwa hawana maslahi ya watu moyoni.

•Lilian amesema hatua ya watu kuwania viti kwa sababu ya umaarufu wao ni jambo la kusikitisha na kudai kuwa ni kiki tu.

Aliyekuwa mpenzi wa gavana Mutua Lilian Ng'ang'a
Image: MERCY MUMO

Bi Lilian Ng'ang'a amewakosoa watu mashuhuri ambao wanajitosa kwenye siasa na kuwania nyadhifa mbalimbali.

Mke huyo wa zamani wa gavana Alfred Mutua amesema watu kama hao kwa kawaida huwa hawana maslahi ya watu moyoni.

"Kwa sababu mtu ni maarufu (kwa sababu yoyote ile) haimaanishi agombee wadhifa. Wengi kama hao hawana nia ya kuwatumikia watu," Lilian alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Lilian amesema hatua ya watu kuwania viti kwa sababu ya umaarufu wao ni jambo la kusikitisha na kudai kuwa ni kiki tu

"Ni kutafuta kikitu.  Inatisha," Alisema.

Lilian alimtema gavana Mutua mwaka jana baada ya kuwa pamoja kwa takriban mwongo mmoja. Kwa  sasa yupo kwenye ndoa nyingine na mwanamuziki Julius Owino almaarufu Juliani.

Juliani anajulikana kuwa mkosoaji wa serikali na tayari amewahi kutoa nyimbo kadhaa akilalamikia uongozi mbaya.

View Comments