In Summary
  • Akiwa kwenye mahojiano msanii huyo alikana madai hayo,huku akiwataka wanamitandao kumpa mama yake heshima
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Muziki Tanzania ya WCB Diamond Platnumz hatimaye amezungumza kuhusu mama yake kumpangia mwanamke wa kuoa.

Uvumi umekuwa ukienea mitandaoni kwamba mama Dangote ndiye amekuwa akimtafutia staa huyo wa bongo mwanamke wa kuoa.

Diamond amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanawake tofauti huku wakiachana baada ya muda, na kubarikiwa na baby mama watatu.

Akiwa kwenye mahojiano msanii huyo alikana madai hayo,huku akiwataka wanamitandao kumpa mama yake heshima.

HUku akizungumzia uvumi huo alisema kwamba hatua ya mama yake kumtafutia mwanake wa kuoa ni jambo la wakati uliopita na wala sio wakati wa sasa.

"Kwanza wanamkosea sana heshima mama yangu, kwa umri wote huu mama yangu hawezi nipangia mtu wa kuoa hayo maisha yashapita zamani sana ya mzazi kukupangia wewe umuoe nani au usimuoe nani, mama yangu hawezi kunipangia," Alisema Diamond.

 

 

 

 

 

View Comments