logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baba yangu alitarajia niwe mtoto wa kiume-Vivianne afichua

"Hatua yangu ni kwamba maisha yamejaa mafunzo mengi ya kujifunza.

image
na Radio Jambo

Habari25 May 2022 - 09:00

Muhtasari


  • Ambapo tunatafuta suluhisho kila wakati nje. Ile stori ya ule aunty/uncle aliku-promise job .. hadi Leo una-wait."
Instagram, KWA HISANI

Msanii Vivianne kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameficua kwamba baba yake alipogundua mama yake ana ujauzito alifikiri kwamba atazaa mtoto wa kiume.

Kulingana na msanii huyo, alipokuwa anakua hakujielewa yeye ni nani, huku akisema kwamba maisha yamejaa mafunzo.

"Haikuwa hivi kila mara. Hivi majuzi niligundua kwamba siku nilipokuja katika ulimwengu huu baba yangu alitarajia mtoto wa kiume alafu kidogo kidogo ni mimi #ViviKamaVivi .

Kama baadhi yenu nilikua sijui mimi ni nani na wazazi wangu walifanya tu kile wanachojua. Alafu si mnajua 8-4-4 ilitufanya ile kitu.

Ambapo tunatafuta suluhisho kila wakati nje. Ile stori ya ule aunty/uncle aliku-promise job .. hadi Leo una-wait."

Aliongeza;

"Hatua yangu ni kwamba maisha yamejaa mafunzo mengi ya kujifunza. Mimi ni mtetezi wa amani ya akili.

Njia pekee ambayo nimefika hapa ni kupitia kujipenda bila masharti. Yaani wakuongea mzidi sana."

Vivian anasema kufanya muziki kumemfanya ajitambue yeye ni nani. Hii ni licha ya hali hasi zinazotokana na kuishi maisha yake ya kifahari.

"Kupitia zawadi yangu ya muziki nimepata kujua mengi kuhusu mimi halisi ( mzuri na si mzuri sana) lakini ni mimi tu.

Imebidi niwe na uthubutu kubaki hapa. Watu wengine wanafikiri ninahitaji kuimba kuabudu wengine wanafikiri nahitaji kufanya nyimbo za mapenzi na nimehukumiwa sana juu ya hili.

Lakini kwangu hakuna makosa katika safari yangu ya muziki na kwa kila mtu ambaye nimemuinua kwa sababu ya zawadi hii namshukuru Mungu."

Vivian aliendelea na ushauri

"Rafiki mmoja aliniambia hakuna hata mmoja wetu ambaye ni maalum zaidi kuliko mwingine ni juu ya kanuni tunazoishi. Kanuni moja kama hiyo ni kwamba mtu pekee anayekuja kukuokoa ni toleo lako lililoponywa.

Kwa hivyo wacha tuponye akili zetu, tufanye kazi kwa afya njema, tusamehe haraka, tuache uzembe na tukumbuke jinsi tunavyojiona ndio jambo pekee ambalo lina maana. #vivithealbamu"


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved