In Summary

•Kate alisema mwanawe amekuwa msukumo wa maisha yake tangu alipomzaa na kuweka wazi kuwa anajivunia maendeleo yake.

•Leon alizaliwa wakati Kate alikuwa anaendeleza masomo yake ya chuo kikuu katika nchi jirani ya Uganda.

Image: INSTAGRAM// KATE ACTRESS, KAMAU

Mwanawe muigizaji Catherine Kamau (Kate Actress) anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi leo (Julai 30).

Leon Kamau ambaye ni mtoto wa kwanza wa muigizaji huyo anatimiza miaka 16.

Kate ametumia fursa hiyo kusherehekea mwanawe kwa ujumbe maalumu kupitia mitandao ya kijamii.

"Kheri za siku ya kuzaliwa mwanangu, nina mengi ya kusema lakini najua ulisema hakuna jumbe ndefu na picha za aibu. Nitaheshimu hilo, wewe mtu mzima mwenye ndevu mbili," Kate aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Muigizaji huyo mwenye kipaji kikubwa aliambatanisha ujumbe wake na picha ya mwanawe ambaye anaonekana mkubwa kweli.

Alisema mtoto wake amekuwa msukumo wa maisha yake tangu alipomzaa na kuweka wazi kuwa anajivunia maendeleo yake.

"Wewe ni motisha wangu toka siku ya kwanza , natumai nimetimiza ahadi zangu kwako , nakupenda sana na ninajivunia wewe hadi sasa 🤗🙏🏽 . Sasa naomba uende maji nyasi ukimaliza osha mabati," Aliongeza msanii huyo.

Image: INSTAGRAM// KATE ACTRESS

Muongazaji wa filamu Philip Karanja, na ambaye ni mume wa Kate pia alimsherehekea mwanawe huyo wa kambo.

"Rasmi huyu Jamaa Ako na ndevu mob kuniliko😩 wadau nipatieni Siri🤷🏾‍♂️ Heri ya siku ya kuzaliwa @kamauuuu_," Phil aliandika kwenye Instagram.

Leon alizaliwa wakati Kate alikuwa anaendeleza masomo yake ya chuo kikuu katika nchi jirani ya Uganda.

Mwaka jana muigizaji huyo alifichua kuwa alipachikwa ujauzito wa kifungua mimba hicho chake  miezi mitatu tu baada ya kujiunga na chuo kikuu cha Kampala.

Kate alikiri kuwa aliponda raha kweli kuanzia siku za kwanza kwanza alipojiunga na chuo kikuu na alishtuka sana wakati daktari alipomvunjia habari kuhusu ujauzito wake.

"Ilikuwa kama uhuru. Ningeweza kuenda nje. Tulikuwa  karibu na Kabaragala, hepi kila wakati.. tulidunda. Hata sikupumua, miezi mitatu nikabeba ujauzito. Sikuelewa jinsi ilikuwa mshtuko kwangu, ilikuja haraka. Hata daktari aliponiambia sikuamini. Nilikuwa msichana mdogo na mtu hangejua. Sikufahamu kuhusu kutumia mbinu za kuzuia ujauzito. Niliendea dawa za 'Morning after' baada ya wiki tatu " Cate alisimulia katika mahojiano na Churchill.

Muigizaji huyo alidai kuwa jamaa aliyempachika ujauzito alimsaidia siku za kwanza lakini baada ya kuona jinsi mambo yalivyoendelea kuwa mazito akamuacha.

View Comments