In Summary

•Robert Ndegwa, almaarufu Thee Pluto amejibu watu wanaomchukia wakimkosoa kwa kununua gari jipya.

•Katika mahojiano na Nicolas Kioko, MwanaYouTube alibaini kuwa baada ya kununua gari hilo jipya, Mazda CX-5, watu wanaomchukia wamekuwa wakimwongelea vibaya Mitandaoni.

Thee Pluto picha/@thee_pluto/Instagram
Image: INSTAGRAM

Robert Ndegwa, almaarufu Thee Pluto amejibu watu wenye chuki wanaomkosoa kwa kununua gari jipya.

Katika mahojiano na Nicholas Kioko, Mwanavlogu huyo alibainisha kuwa baada ya kununua gari jipya aina ya Mazda CX-5 baadhi ya wanamitandao  wamekuwa wakielekeza chuki kwake.

Thee Pluto alidokeza kwamba uamuzi wake wa kupata hilo gari  haukuwapendeza baadhi ya wanamitandao ambao walipendekeza kwamba angefikiria kuwekeza  pesahizo badala ya kununua gari.

Hata hivyo, MwanaYoutube huyo  alibainisha kuwa anayachukulia maneno ya wanamitandao kama changamoto ambazo lazima aelewe.

“Vile niliongeza hii CX-5, kuna watu pale kwa comment section walikua wanasema ‘ooh jenga nyumba kwanza' nani amekuambia sijajenga?

"Wakati fulani, watu hawa wanachukia kupita kiasi na wanaishi chini ya paa za mama zao. Chukua kitu kama changamoto na Mungu atakubariki," Thee Pluto alisema.

Hivi majuzi Thee Pluto alinunua gari, aina ya Mazda CZ-5 2016 ambayo thamani yake sokoni ni kati ya KSh 2.48 milioni hadi KSh 2.98 milioni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Thee Pluto mwenye  umri wa miaka 22 alipost picha akiwa na gari lake mpya.

Asante Mungu. Kwa neema ya Mungu. Mtoto mwingine katika orodha yangu,” Thee Pluto alinukuu picha hiyo.

Mnamo Novemba 2021, Mwana Youtube huyo  alionyesha gari jipya, Toyota Landcruiser TX ambalo alijipa zawadi wakati akiashiria siku yake ya kuzaliwa ya 22.

Akizungumza na vyombo vya habari, Thee Pluto alisema alinunua gari hilo kwa KSh 4 milioni ingawa lilikuwa linamilikiwa awali.

Kichezeo kingine kwa ufalme wangu kabla tu ya sherehe za siku yangu ya kuzaliwa kesho. Land Cruiser (TX) 'Na kumbuka! Mola wenu Mlezi alitangaza: Mkishukuru nitawazidishia. Quran 14: 5-7'," alisema kwenye Instagram.

Land Cruiser (TX) 2016 inagharimu kati ya KSh 4.5 milioni na KSh 7 milioni.

View Comments