In Summary

• Caroline Aturinda alikuwa mwanafunzi katika chuo cha sheria na alitarajiwa kufuzu tarehe 29 Julai.

•Treni lilisomba gari lao kwa kishindo na kumuua yeye na wenzake wawili papo hapo.

Mapema wiki hii, jumuiya ya Afrika Mashariki iliamkia taarifa za kuhuzunisha kuhusu ajali iliyohusisha treni lililogonga gari la kibinafsi nchini Uganda na kuwaua wote waliokuwemo ndani ya gari hilo.

Jambo la kugandisha nyoyo hata zaidi ni kwamba watu watatu waliokuwemo kwenye gari lile walifariki papo hapo baada ya gari lao kugaragazwa na kubondwa kwa kishindo cha garimoshi. Mmoja wao alikuwa mwanafunzi wa sheria ambaye alitajaria kuhafili mwishoni mwa mwezi Julai kulingana na taarifa kutoka chuo alichokuwa akisomea.

"Ni jambo la kusikitisha kuwa tunatangaza kifo cha Aturinda Caroline kilichotokea jana baada ya ajali ya treni katika Tarafa ya Nakawa. Caroline alikuwa mwanafunzi wa LDC na alitarajiwa kuhitimu tarehe 29 Julai, 2022. BWANA na aifariji familia yake katika wakati huu mgumu. RIP Caroline," LDC walichapisha kwenye ukurasa wao wa Twitter.

Taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilifichua kwamba mwanadada huyo kwa jina Caroline Aturinda alikuwa ametarajiwa kuhitimu kama wakili mwishoni mwa mwezi huu wa Julai, kabla ya umauti kumkuta pamoja na Rafiki zake wakitoka usiku wa tafrija.

Ajali hiyo ilitokea wakati ambapo gari hilo lilikuwa linajaribu kupita katika kivuko cha reli na kukutana na gari mosi lililokuwa likija kwa kasi mno kupekelea kulipinga gari kwa dafrau na kuwaua waliokuwemo.

Shirika la reli nchini humo limejiondolea lawama kutokana na ajali hiyo mbaya kwa kusema kwamba dereva wa gari moshi alipiga honi mara kadhaa kama ilivyo kadhia kabla ya kufika kwenye kivuko hicho lakini ni kama dereva wa gari dogo hakutilia maanani na kupelekea gari lake kusombwa na kasi ya treni.

Kwa upande wa chuo cha wanasheria alichokuwa akisoma mwanadada Caroline waliitaka mamlaka husika kuweka vidhibiti halisi vya treni katika maeneo ya kuvukia magari ili kuepusha ajali kama hizo siku za mbeleni.

View Comments