In Summary
  • Huku akinakili ujumbe kwa mwanawe Ruth alifichua jinsi mwanawe alifuta machozi yake, na kumpa sababu nyingine ya kuishi
MSANII WA NYIMBO ZA INJILI RUTH MATETE NA MWANAWE
Image: RUTH MATETE/INSTAGRAM

Msanii maarufu wa nyimbo za injili Ruth Matete kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemsheherekea mwanawe kwa ujumbe wa kipekee.

Ruth aliandika ujumbe huo huku akisheherekea siku ya kuzaliwa na mwanawe.

Huku akinakili ujumbe kwa mwanawe Ruth alifichua jinsi mwanawe alifuta machozi yake, na kumpa sababu nyingine ya kuishi.

Msanii huyo pia amesema kwamba maisha yake yalibadilika baada ya kupata baraka zake ambazo ni mwanawe.

"Heri njema siku ya kuzaliwa  binti yangu,Ikiwa nitaanza kuandika kitabu juu ya jinsi maisha yangu yamebadilika tangu nilipokutana nawe, sitaweza kumaliza

Mwanangu, umenifuta machozi. Ulinipa sababu ya kutaka kuishi tena.

Wewe ni msukumo wangu mkuu. Unaangazia siku zangu kama hakuna mtu aliyewahi kufanya.

Unapofikisha miaka miwili leo, jua kwamba mummy anakupenda sana!Maisha marefu ni sehemu yako katika jina la Yesu Kristo!"Ruth Aliandika.

Wanamitandao walimtakia mwanawe Ruth heri njema ya siku ya kuzaliwa na hizi hapa baadhi ya jumbe zao za kufana;

sandra_dacha: Happy birthday baby gal😍

perislucky: Wow mummy and baby looking all glamorous happy birthday baby you will love to tell of the goodness of God ❤️

favour_mumbi: Happy birthday Toluwa May God bless and keep you and make His face shine upon you always ❤️ you are blessed of the Lord❤️well done ma.a

wambui_kimotho: Happy birthday baby Toluwa. With long life and favour with Him and men, may the Lord satisfy you with❤️.

 

View Comments