In Summary

• Diamond Platnumz yuko safarini kuelekea Qatar kushuhudia baadhi ya mechi zilizosalia za Kombe la Dunia.

•Ziara ya wawili hao ilidhaminiwa na kampuni ya kamari ya Diamond, Wasafi Bet.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa Bongo Diamond Platnumz yuko safarini kuelekea Qatar kushuhudia baadhi ya mechi zilizosalia za Kombe la Dunia.

Siku ya Jumatatu mkurugenzi huyo wa Wasafi Bet alichapisha picha iliyomuonyesha akiwa ndani ya ndege la kuelekea katika nchi hiyo ya Asia. Alikuwa ameandamana na msemaji wa Yanga S.C Haji Manara.

Safari ya Diamond na Manara pia ilitangazwa kupitia ukurasa rasmi wa lebo ya WCB.

"Safari kwenda Qatar #FIFAWORLDCUP," taarifa iliyoandikwa chini ya picha ya Diamond na Manara ilisoma.

Ziara ya wawili hao ilidhaminiwa na kampuni ya kamari ya Diamond, Wasafi Bet.

Diamond na Manara wanaelekea Qatar huku mashindano ya Kombe la Dunia bado yakiwa katika hatua ya kwanza ya makundi.

Mataifa matano; Ghana, Tunisia, Morocco, Cameroon na Senegal ndiyo yanawakilisha bara Afrika katika mashindano hayo. Hakuna taifa lolote la Afrika Mashariki ambalo linashiriki kwenye mashindano hayo.

Kabla ya Kombe la Dunia kuanza, Diamond ali tangaza ofa maalum kwa mashabiki wa kandanda wanaoweka dau kupitia Wasafi Bet.

Kampuni ya  Wasafi Bet ilizindua promosheni ya Twende Qatar Na WasafiBet katika hafla iliyoandaliwa Milimani City.

Promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na mkurugenzi wa kampuni, Diamond ilitoa nafasi kwa washiriki kamari wanaoweka dau la zaidi yaTsh 2000 (Ksh100)  kujishindia tiketi ya ndege ya kwenda Qatar kushuhudia moja kwa moja mashindano ya kombe la dunia yatayoendelea hadi Desemba 18.

"Leo rasmi mkurugenzi wa wasafibet Bw Diamond Platnumz amefungua promosheni mpya iitwayo Twende Qatar na Wasafibet ambayo ukibashiri kwa 2000 tu unapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuwania tiketi ya kwenda Qatar," WasafiBet ilitangaza  kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Wengine waliokuwepo wakati wa uzinduzi huo ni pamoja na mamake Diamond Mama Dangote Zuchu, Baba Levo, Mwijaku, H-Baba, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James pamoja na wageni wengine wakuu.

View Comments